RAIS WA SINGIDA FOUNTAIN GATE AITISHA KIKAO CHA DHARURA

Rais wa Klabu ya Singida Fountain Gate amekutana na wachezaji na benchi la ufundi kujadili mwenendo wa timu na kuweka mikakati imara kwenye Mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kikao kimelenga kuimarisha ufanisi wa timu baada ya matokeo mabaya katika mechi za karibuni. Singida Fountain Gate, ambayo haijapata matokeo mazuri hivi karibuni, inaonyesha uongozi thabiti na jitihada za kuchukua hatua za haraka kurekebisha mwenendo. Uamuzi wa kufanya kikao na wachezaji na benchi la ufundi unathibitisha dhamira ya uongozi wa klabu hiyo katika kuboresha utendaji wao uwanjani. Hatua hii inaonyesha mfano wa uongozi bora wa Japhet Makau; Rais na mmiliki wa Klabu, ambaye anajitahidi kusimamia timu yake katika nyakati nzuri na mbaya. Singida Fountain Gate inaweka misingi imara ya kufanikiwa katika mzunguko wa pili ikiwa imebakiza mechi 14 za kumalizia msimu wa Ligi Kuu NBC na kuimarisha imani ya mashabiki na wadau wengine. Bado hawajachelewa. Mechi 14 zinatosha kuwafikisha kwenye malengo yao msimu huu ikiwemo kupata nafasi ya kushiriki tena michuano ya kimataifa.

Singida Big Stars

Share

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

go top